January 4, 2016


Uongozi wa benchi la ufundi la Yanga umempa cheo cha unahodha, kiungo wa timu hiyo Mbuyu Twite baada ya Haruna Niyonzima kuondoka klabuni hapo.

Awali kabla ya Niyonzima ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda kupewa wadhifa huo cheo hicho kilikuwa mikononi mwa Twite, hivyo hii ni mara ya pili kwa kiraka huyo kuchukua nafasi hiyo.

Twite anatazamiwa kutumia nafasi hiyo kuiongoza Yanga kwenye michezo yote ya Kombe la Mapinduzi na ile ya awali baada ya kurejea kwa Ligi Kuu Bara kutokana na nahodha mkuu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuwa majeruhi.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema kuwa cheo hicho kipo kwa Twite kwa muda tu kwa kuwa bado benchi la ufundi chini ya Mholanzi, Hans van Der Pluijm, halichagua nahodha msaidizi mpaka sasa.


“Twite kwa sasa ndiyo anaongoza timu kama nahodha msaidizi baada ya Niyonzima kuondoka, ila atafanya hivyo kwa muda maana bado hajateuliwa nahodha mpya msaidizi atakayesaidiana na Cannavaro,” alisema Saleh.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic