Kiungo Haruna Niyonzima aliyetupiwa virago na Yanga amesema bado hajapewa barua, jambo linalomfanya asijue nini cha kufanya na ugumu kuhamia timu nyingine.
Niyonzima alivunjiwa mkataba wake na Yanga kutokana na kile uongozi wa timu hiyo ulichodai mchezaji kukiuka vipengele vya mkataba wake ikiwemo ya kuchelewa kurejea ndani ya kikosi hicho akitokea nchini kwao.
Niyonzima alisema hadi sasa hajui afanye nini ama aamue nini juu ya muelekeo wake kwa kuwa licha ya kupata taarifa ya kuachwa na klabu yake hiyo lakini hadi sasa wapo kimya katika kumkabidhi barua yake ya kutimuliwa ndani ya kikosi hicho.
“Kwa kweli sielewi na wala sijaamua kitu chochote hadi sasa juu ya mwelekeo wangu wa maisha ya soka kwa kuwa bado Yanga hawajanipa barua yangu hivyo inakuwa ni vigumu kupanga mambo yangu mengine.
“Nitakapoipata barua ndipo nitakapoweza kuamua nini cha kufanya na kwa sasa siwezi kuzungumzia suala hilo kiundani hadi nitakapopewa taarifa rasmi ya mimi kuondolewa ndani ya timu hiyo,” alisema Niyonzima.
0 COMMENTS:
Post a Comment