January 15, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo akiwaambia: Tulieni mtauona mziki wa Mniger, Issoufou Boubacary.

Mniger huyo anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alitua kuichezea timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu Bara akisaini mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Mbrazili, Andrey Coutinho.

Mshambuliaji huyo, hadi hivi sasa amecheza mechi mbili pekee, moja ya ligi kuu dhidi ya Mbeya City na nyingine dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Kombe la Mapinduzi, ambapo alifanikiwa kupachika bao moja.

Pluijm alisema, ni ngumu kumbeza mshambuliaji huyo hivi sasa, badala yake anahitaji kupewa muda kwa ajili ya kubadilika, ndiyo maana anamfuatilia kwa jicho la ziada ili kuona maendeleo yake kila siku.

Pluijm alimtolea mfano Mtogo, Vincent Bossou, akisema hakuwa kwenye ubora wake awali lakini baada ya muda uwezo wake ukaanza kuonekana na sasa ni tegemeo katika kikosi cha kwanza.

“Sipendi kumzungumzia mchezaji mmojammoja, lakini kwa hili la Boubacary ningependa kulizungumzia kwa kusema kuwa anahitajika kupewa muda kwa ajili ya kuangalia uwezo wake.


“Ninaamini kadiri siku zitakavyokwenda ndiyo kiwango cha mchezaji huyo kitabadilika, kama ilivyokuwa kwa Bossou,” alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic