Kamati iliyokuwa ikisimamia michuano ya Kombe la Mapinduzi, imetakiwa kuwa makini katika uchaguzi wa timu shiriki ili kuongeza nguvu ya ushindani.
Kocha wa URA, Fredi Munjunsi, ambaye timu yake ndiyo iliyotwaa ubingwa wa michuano hiyo juzi, alisema wanatarajia kurejea mwakani kutetea ubingwa wao lakini akashauri kuwa kamati inatakiwa kuzikaribisha timu zenye changamoto kubwa na siyo ilimradi zishiriki tu kwenye michuano.
“Kunatakiwa kuwe na timu zenye ushindani mkali na siyo zishiriki tu bila kuwa na msaada, kama tulivyo sisi, tumekaribishwa na tumetwaa ubingwa,” alisema kocha huyo.
Wakati huohuo, Mtibwa Sugar ambayo imeshika nafasi ya pili katika michuano hiyo, kocha wake Mecky Maxime amedai kuwa tatizo hawakuwa na bahati.
"Imeniuma sana kwani tunajiona kama tuna bahati mbaya ya mashindano haya, kwa sababu tumetinga fainali mara tano lakini ni mara moja tu ndiyo tuliyofanikiwa kuibuka mabingwa. Tulicheza vizuri sana mwaka huu, tunarudi nyumbani kujipanga,” alisema Maxime.
MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI
Mwaka Bingwa Wa Pili
2007: Yanga Mtibwa
2008: Simba Mtibwa
2009: Miembeni KMKM
2010: Mtibwa Ocean View
2011: Simba Yanga
2012: Azam Jamhuri
2013: Azam Tusker
2014: KCCA Simba
2015: Simba Mtibwa
2016: URA Mtibwa
0 COMMENTS:
Post a Comment