January 8, 2016


Baada ya zile vurugu kali katika mechi ya Kombe la Mapinduzi, mshambuliaji Donald Ngoma wa Yanga na beki Serge Wawa wa Azam FC, wamefanya kikao cha muda.

Kikao hicho kilifanyika kikiongozwa na Thabani Kamusoko, kiungo raia wa Zimbabwe ambaye alionekana kutofurahishwa na ugomvi uliotokea wakati wa mechi hiyo tangu mwanzo.

Kamusoko alishirikiana na beki Mtogo, Vincent Bossou kuzungumza na Ngoma na Wawa ili kuwapatanisha.

Kikao hicho kilifanyika kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar katikati ya uwanja mara tu baada ya mpira kwisha na wanne hao walizungumza kwa dakika kadhaa kabla ya Ngoma na Wawa kupeana mikono kuonyesha mambo yalikuwa yamekwenda “mswano”.

Vurugu za wachezaji kukamiana, kukabana, kutemeana na kutwangana zilitokea kwa wingi katika mechi hiyo ya Kombe la Mapinduzi.

Wawa na Ngoma walivurugana vibaya baada ya Wawa kumchapa Mzimbabwe huyo kibao. Hasira za Ngoma, ilikuwa ni kulipiza kwa kumkaba beki huyo raia wa Ivory Coast kama alikuwa akitaka kumuua.

Kukamiana katika mechi hiyo ya Kombe la Mapinduzi kwa Kundi B inaonyesha upinzani wa Yanga dhidi ya Azam FC unavyozidi kupanda kwa kasi.


Matokeo yake yalikuwa ni sare ya bao 1-1 huku Azam FC ikitangulia kufunga kupitia Kipre Tchetche kabla ya Yanga kusawazisha, shujaa wao akiwa Bossou.

1 COMMENTS:

  1. Kweli mnawapenda Azam, Simba na Yanga wakifanya vurugu ni kuuwa mpira ila Azam wakifanya ni kukua kwa upinzani!! HAhahaga Siasa kwenye soka.......!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic