January 9, 2016


Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure amepinga uamuzi wa Caf kumpa tuzo ya mwanasoka bora Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund na Gabon.

Toure anasema yeye ndiye anastahili kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya nne kutokana na kiwango chake Ulaya lakini pia kufanya vizuri kwa Ivory Coast ambao ni mabingwa wa Afrika na yeye akiwa nahodha.

Toure ametoa dukuduku lake hilo mara baada ya Aubameyanga kushinda tuzo hiyo jijini Lagos nchini Nigeria juzi.

Toure aliyebeba tuzo hiyo mara tatu mfululizo alishika nafasi ya pili na tatu ikaenda kwa Andre Ayew wa Ghana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic