February 15, 2016

AFRICA LYON ILIYOKUWA LIGI KUU KABLA YA KUPOROMOKA

African Lyon ya jijini Dar, jana Jumapili ilifanikiwa kurejea tena ligi kuu, kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya Ashanti United katika mchezo wa mwisho wa Ligi Daraja la Kwanza uliyopigwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar.

Lyon imemaliza Kundi A ikiwa kileleni kwa pointi 27, ikifuatiwa na Ashanti yenye 24 huku Friends Rangers ikishika nafasi ya tatu baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Kiluvya United katika mchezo wao uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, jana.

Lyon inaungana na Ruvu Shooting kutoka Kundi B, huku kitendawili kikibaki kwa Kundi C baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusema halitaitangaza timu iliyopanda ligi kuu kati ya Geita Gold Sports na Polisi Tabora mpaka pale litakapopata ripoti ya waamuzi wa michezo hiyo kutokana na jinsi matokeo yake yalivyokuwa na utata.


Mbali na timu zilizopanda, kwa upande wa pili, timu za Mji Mkuu kutoka Dodoma, Burkinafaso (Morogoro) na JKT Kanembwa ya Kigoma zimeshuka daraja kutoka ligi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic