February 15, 2016


Pamoja ya viungo wa Simba, Mzimbabwe, Justice Majabvi na Jonas Mkude kuonekana muhimili mkubwa wa kikosi cha Simba kwa sasa, kiungo wa kimataifa wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amesema kwake anawaona ni wachezaji wa kawaida tu.

Hiyo imekuja ikiwa zimesalia siku tano pekee kabla ya mechi baina ya wababe hao itakayopigwa Februari 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo fukuto la mchezo huo limeshaanza kuwagubika mashabiki wa timu hizo mpaka wachezaji wenyewe.

Niyonzima ambaye juzi Jumamosi alifanikiwa kuiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim SC ya Mauritius, pia ameelezea jinsi anavyoelewana na kiungo mwenzake, Mzimbabwe Thabani Kamusoko pale inapotokea wamepangwa pamoja, hivyo anaamini watafanya kazi nzuri.

MAJABVI

“Naweza kusema mechi ya Simba ni ngumu ila kwa upande wetu wachezaji tunajiandaa vizuri kwa ajili ya kufanya kazi yetu vizuri na mwisho wa siku tuibuke na ushindi katika hiyo mechi, Mkude na Majabvi naona ni wa kawaida tu, nafikiri tusubiri tutaona siku ya mechi.

“Kombinesheni yangu na Kamusoko ni nzuri kwa sababu tunajuana muda mrefu, kwa hiyo inakuwa rahisi kuelewana tukiwa uwanjani,” alisema Niyonzima.

Siku chache zilizopita, Mkude aliwahi kunukuliwa akiionya Yanga kuelekea katika mchezo wao huo akiitahadharisha kuwa makini kutokana na uimara na spidi waliyonayo kwa sasa katika kushinda mechi zao mfululizo za Ligi Kuu Bara.  



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic