February 5, 2016

MGAMBO SIMBA WALIVYOPAMBANA...

Bao la dakika ya 88 lililofungwa na straika wa Mgambo Shooting, Fully Maganga, juzi Jumatano liliweka rekodi tatu tofauti kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Maganga alifunga bao hilo la kufutia machozi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara wakati Mgambo ilipokubali kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Simba.

Rekodi ya kwanza ni ile ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Mgambo kufunga bao kwenye uwanja huo kwani kabla ya hapo wachezaji wa kikosi hicho hawakuwahi kupata bao lolote katika uwanja huo tangu timu hiyo ilipopanda daraja misimu minne iliyopita.

Rekodi ya pili, kipa wa Simba, Vincent Angban alikuwa hajafungwa bao katika dakika 538 mfululizo, lakini rekodi yake hiyo ikaharibiwa na straika huyo huku akivunja nyingine ya mwisho kwa Kocha wa Simba, Jackson Mayanja ya kuiongoza timu hiyo kucheza mechi nne mfululizo bila ya kufungwa.

Mayanja, tangu aanze kuinoa Simba amefanikiwa kuiongoza kucheza mechi tano ambazo moja kati ya hizo ndizo ameruhusu bao lakini zote ameibuka na ushindi.


Matokeo ya mechi hizo yalikuwa hivi; Simba 1-0 Mtibwa, Simba 2-0 JKT Ruvu, Simba 4-0 African Sports, Simba 5-1 Mgambo ambazo hizo zote ni za ligi huku ikiifunga Burkinafaso mabao 3-0 kwenye Kombe la FA. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic