MPIRA UMEKWISHAAAA...
DAKIKA TATU ZA NYONGEZA
KADI NYEKUNDU Dk 90 Daud Jumanne wa Kagera analambwa kadi nyekundu, haijajulikana tatizo lilikuwa nini pale
Dk 89, Kagera wanafanya shambulizi kali langoni mwa Simba lakini Banda anajitahidi kuokoa
Dk 81, Lyanga anauwahi mpira katika eneo la hatari lakini Kagera wanaokoa
Dk 76, Iddi Kurachi anapiga ule mpira, unawababatiza mabeki wa Simba. Wanawahi na kuokoa
KADI Dk 75 Banda anafanya uzembe, Ally anamtoka anamshika na mwamuzi anamlamba kadi ya njano. Mpira utapiga nje kidogo kwenye kona ya boksi ya 18, tusubiri
Dk 73, beki wa Kagera anajichanganya mpira unamkuta Lyanga nje ya 18 anapiga shuti kali, linamgonga beki wa Kagera, inakuwa kona. Simba wanapiga inakuwa haina madhara
Dk 71, Kanoni anarusha mpira langoni mwa Simba unatolewa na Juuko na kuwa kona, anaichonga mwenyewe lakini haina madhara kwa Simba
SUB Dk 67, Simba inamtoa Kiiza, nafasi yake inachukuliwa na Bryan Majegwa
Dk 64, krosi nyingine safi kwa Kiiza, yeye na kipa anapasiha tena
Dk 60, Kiiza anapoteza nafasi ya nne, kazi nzuri ya Kazimoto kuwatoka mabeki wawili na kutoa pasi nzuri, hatua mbili kutoka lango la Kagera anapaisha buuuuu
Dk 58 hadi 59, kiazi Kagera wanaamka na kuanza kugongeana vizuri
Dk 57, krosi ya Kanoni, inamkuta Kavila anapiga shuti kali, unatoka nje kidogo ya lango la Simba. Hii inaonyesha Simba lazima wawe makini
SUB dk 56 Simba inamtoa Ugando na nafasi yake inachukuliwa na Danni Lyanga
Dk 55, nafasi nzuri kabisa Ugando, Ajib anawachambua mabeki na kumpa krosi nzuri kabisa, anatoa nje
Dk 50, krosi safi ya Kessy, Kiiza anaukosa mpira hatua mbili kutoka lango la Kagera. Huenda alifunga macho
Dk 47, Ajib anapiga mkwaju safi wa adhabu lakini Ntalla anaokoa na kuwa kona, lakini haina madhara
MAPUMZIKO
GOOOOOOO Dk 45, Ajib anaifungia Simba bao safi kabisa
Dk 35 hadi 40, mpira umepooza, hauna mashambulizi mengi na hakuna timu inayoshambulia zaidi na kupeleka hatari nyingi langoni kwa mwenzake
Dk 34, krosi nzuri ya Tshabalala inamfikia Kiiza, baada ya kufunga anampa Ugando, naye anampa mikononi kipa Ntalla
KADI Dk 29, George Kavila analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Kazimoto
Dk 24, Kazimoto, Ajibu wanagongeana vizuri, pasi inamfikia Kiiza, anapiga na mpira unatoka sentimeta chache kwenye lango la Kagera
Dk 21, Kessy anapiga krosi nzuri, lakini Ntalla anakuwa na spidi kuliko Ajib, anauwahi mpira
Dk 9, Ajib anamtoka beki wa Kagera katikati ya lango, anaingia na kutoa krosi lakini inakuwa haina mwenyewe
Dk 5, Ajib anaingiza krosi nzuri lakini Ntalla anawahi na kuudaka
Dk 3 zinakatika bila timu yoyote kugusa lango la timu nyingine
Dakika moja yote inachezwa bila ya timu yoyote kugusa lango la mwenzake

Mwamuzi wa mchezo ni Mathew Akrama
0 COMMENTS:
Post a Comment