February 29, 2016


Beki wa Simba, Hassan Ramadhan Kessy, amegomea mkataba wa timu hiyo baada ya ule wa awali kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu huku akiutaka uongozi wa timu hiyo kumpa milioni 60 ndiyo akubali kuanguka saini.

Kessy ambaye alisajiliwa Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akitokea Mtibwa Sugar ambapo kumekuwa na vuta nikuvute baina yake na klabu yake hiyo tangu atue katika timu hiyo, awali aligoma kucheza kutokana na kutopewa nyumba na kutomaliziwa fedha za usajili.

Hata hivyo, mchezaji huyo ameonekana kuendelea kuwatesa viongozi wa Simba kutokana na kumhitaji mchezaji huyo huku akionyesha kuwa ni wa gharama kubwa.

Chanzo cha kuaminika kutoka Simba kimeeleza kuwa, Kessy amewataka viongozi wa timu hiyo kumpa kiasi cha shilingi milioni 60 ili aweze kuanguka saini ya kuendelea kuitumikia timu hiyo, jambo ambalo limewashinda viongozi.

Aidha, inadaiwa kuwa dau hilo kubwa analolitaka mchezaji huyo linachangiwa na tetesi kuwa klabu kubwa za Yanga na Azam FC kumnyemelea hivyo kuwapa ugumu.

“Awali viongozi wa Simba walimuita Kessy ili aweze kuanguka saini, akakataa, hivyo kuleta mvutano na kutaka alipwe milioni 60, kiasi ambacho uongozi hauna uwezo nacho kulingana na hali halisi ya klabu kwa sasa.

“Uongozi unaendelea na mazungumzo na meneja wa Kessy, Athuman Tippo kuona watafikia wapi kwani kiasi cha fedha kilichopo ni kidogo na iwapo itashindikana basi tutaachana naye na kutafuta mbadala wake,” kilisema chanzo hicho.

Simu ya Kessy haikupatikana hewani kwa muda wote tangu juzi na jana hakuwepo hata benchi katika kikosi kilichocheza Kombe la FA dhidi ya Singida United.


2 COMMENTS:

  1. Nafikiri aina hii ya uandishi si sahihi.Ni kitu gani kilichonuka hapo,mbona nimefuatilia andiko lako sikuona mahali popote kwenye hilo bandiko ambapo pana harufu ya mnuko uliousema?Kumalizika kwa mkataba wa awali kunatoa fursa kwa pande mbili husika kukaa mezani na kujadiliana mkataba mpya kwa kuzingatia mahitaji ya kila upande.Yanayoendelea ni majadiliano juu ya mkataba mpya,wasipoafikiana katika hilo hakuna ugomvi wala upande utakaomlaumu mwenzake,sasa kuna haja gani ya kutoa andiko la kizushi as if kuna mgogoro wa kimkataba? Au unafurahishwa na migogoro ya timu zetu za Tanzania kiasi cha kutoa andiko linaloashiria uwepo wa mgogoro wakati hakuna mgogoro wowote? Kweli Tanzania tuna safari ndefu kuyafikia Maendeleo tunayoyatamani.Kwa aina hii ya uandishi,sidhani kama tunalisaidia soka letu.

    ReplyDelete
  2. Acheni kuhangaika na kufikiria jinsi ya kupata pesa kwa njia haramu,wewe copy & paste link ifuatayo baadae jisajili na kuanza kupiga mahela ukiwa na mtandao wako tuu.Huhitaji kutoa dhamana ya kitu chochote zaidi ya kuwatumia uwapendao hiyo link nao wafaidike.Link yenyewe ni:-http://InvitenShare.com/?ref=65321

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic