February 27, 2016


Na Mwandishi Wetu
WIKI iliyopita, Kampuni ya Multichoice Tanzania ilitangaza habari njema kwa watumiaji wa ving’amuzi vyake vya DStv kwa kuzindua chaneli mpya za michezo zilizowekwa kwenye kifurushi maalum kwa ajili ya kuwafikia wateja wake wote.

Chaneli hizo murua zitakazotambulika kama SuperSport 11 na SuperSport 12 zimezinduliwa rasmi leo kupitia kifurushi kipya cha Compact ambacho sasa kitapatikana kwa Sh 84,500 lakini kwa upendeleo wa mteja mpya atakayenunua king’amuzi hicho atazawadiwa ofa ya bure ya kifurushi cha Compact kwa muda wa mwezi mmoja.
 

Hii itakuwa furaha mpya kwa wapenda soka nchini na michezo mingine. Wale kipenzi cha soka ndiyo walikuwa wakilalamika kutokana na bei huku Multichoice nayo ikilalamika kuishi katika nyakati ngumu kiuchumi kutokana na soko la dunia.

Safari hii, kampuni hiyo ikaamua moja tu na si zaidi. "Kuwashuruku wateja wake" kwa kuendelea kuwa nayo pamoja wakiiunga mkono siku zote.

Multchoice, ikaamua kuingiza ofa hizo ambazo lengo ni shukrani bila ya gharama za ziada. Unaweza kusema kampuni hiyo imeamua kusikiliza tokea moyoni malalamiko ya wateja wake hao kwa kutoa ofa hiyo isiyokuwa na mfano.
 


Akifafanua kuhusiana na hilo, Kaimu Meneja Mkuu wa DStv, Francis Senguji amesema chaneli hizo zinakuja na utamu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Ligi Kuu ya England, Ligi Kuu ya Hispania pamoja na michuano ya Mataifa ya Ulaya 2016.

“Ni katika kutambua hali na nyakati ngumu ya kiuchumi tuliyonayo kwa sasa, tunaelewa pia mahitaji ya wateja wetu na kwa kuzingatia hilo tumeamua kuwasogezea karibu ligi kubwa zote za Ulaya za England na Hispania kupitia kifurushi cha Compact kinachopatikana kwa 84,500 tu.

“Endapo utafanikiwa kuchukua kifurushi hicho mapema faida za awali unazoweza kufaidika nazo kwenye soka ni pamoja na kushuhudia mechi kali za wikiendi hii kule Uingereza kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal, Leicester City na Sunderland na nyingine nyingi.
 


“Hispania pia kutakuwa na ‘game’ kali kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid wakati Barcelona ikivaana na Sevilla na Valencia inayoongozwa na Gary Neville itaingia dimbani kupambana na Athletic Bilbao,” anasema Senguji na kuendelea:

“Kama utazungumzia michezo kwa upande wa soka, basi hakuna kama Premier League na La Liga. Baada ya hapo nyingine zinafuatia. Ving'amuzi vya DStv ndiyo kiboko katika hilo na hakuna mjadala.”

Ofa hiyo sasa inawapa nafasi wapenda soka nchini nao kuweza kuziona ligi hizo ghali kwa kiwango ambacho hakuna anayeweza kulalamika. Tena ikiwezekana kila mmoja anaweza kuangalia mechi hizo akiwa sehemu anayotaka, mfano nyumbani kwake.

Huenda pia ni wakati mzuri wa kuona Multichoice Tanzania ni wasikivu na watu wanaofuatilia wateja wao wanataka jambo lipi. Kwani mara kadhaa kumekuwa na malalamiko kuhusiana na bei.

Ofa hiyo inaonyesha walikuwa wakifuatilia kila jambo, pale walipoona wateja wao wanaumia au kutofurahishwa, nao wakaamua kulifanyia kazi suala hilo na sasa kila mtu anaweza kuwa na furaha.

Kikubwa kwa wateja waliokuwa na ndoto au hamu ya kupata ving'amuzi hivyo ni kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanavipata na kukata kiu yao ya muda mrefu.

Naye Meneja Masoko wa Mulichoice, Furaha Samalu alielezea namna ambavyo wameongeza huduma mpya ndani ya kifurushi hicho cha Premium zikiwemo Express US (Marekani), DStv Now na Box office pia Catch Up.

Taarifa zimeeleza wadau wengi wa soka, wameonyesha kufurahishwa na uamuzi huo wa Multichoice ndiyo maana kuanzia juzi na jana wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kununua ving'amuzi kwenye ofisi ya makao makuu ya kampuni hiyo pamoja na sehemu za mawakala wao nchi nzima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic