February 22, 2016


Wachambuzi wa masuala ya soka nchini England, wameishauri Arsenal kushambulia huku ikimpa kashkash kiungo Sergio Bosquet ili iishinde Barcelona.

Ushauri huo umeendana na kuitaka Arsenal kuachana na kujilinda muda mwingi ikiwa katika lango lake kwa kuwa ni kazi kuwadhibiti washambuliaji watatu hatari wa Barcelona, Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez.

Arsenal itakuwa uwanjani kesho kuwavaa Barcelona katika mechi ya Ligi ya Mabingwa inayotarajia kutazamwa na mashabiki wengi zaidi kuliko nyingine zote msimu hadi sasa.


Barcelona inaonekana kuwa mwiba kwa kila timu kipindi hiki na inaonekana kuwa timu isiyofungika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic