February 22, 2016


Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuendelea wiki hii mzunguko wa nne katika hatua ya 16 bora, kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.

Jumatano Februari 24, 2016 kutakua na mchezo mmoja tu, ambapo timu ya Young Africans watawakaribisha maafande wa JKT Mlale kutoka mkoani Ruvuma katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mchezo utakaochezwa majira ya saa 10:30 jioni.

Michezo miwili itachezwa siku ya Ijumaa ambapo, Ndanda FC watakua wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Nagwanda Sijaon mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Jumamosi Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, wakati jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo.


Mzunguko huo wa nne utakamilika siku ya Jumapili ambapo, Simba SC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

2 COMMENTS:

  1. Nakubaliana nawe kabisa ile faulo ya Banda ilikua fair charge na alisukumwa kwa bega, lakini chunguza faulo ingine half ya pili, iliyofanywa na beki Mbuyu Twite akimchezea Mohammed Hussein, Twite aliachwa na Tshabalala mpira ukawa zaidi ya mita mbili mbele na akawa anamuacha kwa kasi alichofanya na kila mtu aliona, Twite akamkata bila mpira tena rafu inayofikia magotini. Hata kumuonya kwa mdomo hakuonywa, hii nimeiona kwa Josilina tu. Labda na yenyewe ni kosa la kibinadamu.

    ReplyDelete
  2. Ulichokiandika hapo juu ni sahihi sana....angalia kwa makini kabla ya kile kinachoitwa rafu aliyoicheza Abdi Banda nyuma yake tu kidogo Ngoma alimsukuma mtu na wala refa hakuangaika na jambo hilo, ila alikuja kuona tu rafu ya Banda...sasa ukiangalia tukio la Ngoma na la Banda ni kama hakuna tofauti sana..hata hivyo bado refa alikuwa na nafasi ya kumuonya Banda kwa kuwa alishampa kadi ya kwanza halali,kwa kumuonya kwa maneno ingesababisha hata benchi la ufundi la Simba kumtazama Banda kwa jicho la tatu na kama ingewezekana hata kufanya Sub, hivi ndivyo tunavyoona kila siku kwenye ligi za wenzetu huko Ulaya...Vinginevyo basi Wayne Rooney angekuwa anapewa kadi kila mechi....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic