Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars imewasili leo saa 8:30 ikitokea nchini Chad ambako ilitoa kipigo kwa wenyeji.
Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi ngumu kabisa dhidi ya Chad, bao lililofungwa na nahodha wake, Mbwana Samatta. Mechi hiyo ni kuwania kufuzu kucheza michuano ya Afcon.
Akizungumza Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa alisema: "Chad ni wazuri lakini tuliwazidi maarifa."
Pia aliwataka wachezaji wake kuwa makini na mechi ya marudiano kwani timu hiyo ilishawahi kuifunga hapa nyumbani.
"Wana timu nzuri na kamwe hatuwezi kubweteka, tunajua wana timu nzuri na tumepanga kuongeza uhakika," alisema Mkwasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment