March 21, 2016


Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea kujifua mjini N’Djamena kikiwasubiri wenyeji Chad, keshokutwa.

Stars inaivaa Chad katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika, huku ikiwa na matumaini makubwa.Nahodha wake, Mbwana Samatta ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwasili Chad akitokea Ubelgiji ambako anakipiga katika klabu ya KRC Genk.


Hata hivyo, bado kundi moja litajiunga na wenzao kesho akiwemo Thomas Ulimwengu ambaye anatokea DR Congo ambako anaitumikia klabu ya TP Mazembe.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV