March 21, 2016

MAYANJA NA ISIHAKA
Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja ameng’aka kuwa hataacha hata mchezaji mmoja asiye na nidhamu ndani ya kikosi hicho kama itafikia siku ameondoka.

Mayanja raia wa Uganda ameingia kwenye mtafaruku na beki wake Abdi Banda ambaye aligoma kwenda kupasha misuli baada ya kutakiwa kufanya hivyo na kocha huyo wakati Simba ikiivaa Coastal Union mjini Tanga, juzi.

Katika mechi hiyo, Simba ilishinda kwa mabao 2-0 lakini Banda alikataa kupasha misuli ili aingie kuchukua nafasi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

BANDA
“Siwezi kukubali kuwe na mchezaji mkubwa kuliko kocha, sitatoa nafasi kwa mchezaji kuwa mkubwa kuliko klabu,” alisema Mayanja alipoulizwa kuhusiana na suala la yeye kutofautiana na Banda, juzi.


“Mimi ni kocha, ninapokueleza lazima ujue nina maanda yangu. Vipi akatae kuingia. Nakuhakikishia hili sitakubaliana nalo, siwezi kuacha hata mchezaji mmoja asiye na nidhamu ndani ya klabu hii,” alisema kwa msisitizo.

Hivi karibuni, aliyekuwa nahodha msaidizi wa Simba, Hassan Isihaka ambaye aligoma kupangwa katika mechi dhidi ya Singida United.

Baada ya hapo, Mayanja zaidi alikuwa akimtumia Banda katika nafasi aliyokuwa akicheza Isihaka hadi Banda alipolambwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Yanga.

Mechi hiyo alimuingiza Novatus Lufunga ambaye hadi sasa amekuwa tegemeo katika nafasi hiyo akisaidiana na Mganda, Juuko Murshid.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic