March 21, 2016


Unaweza kusema hii ni kasheshe baada ya beki Abdi Banda kuingia katika mgogoro mkubwa dhidi ya kocha wake, Jackson Mayanja.

Taarifa zinaeleza, Banda aligoma kuingia wakati alipotakiwa kufanya hivyo wakati wa mechi dhidi ya Coastal Union ambayo Simba ilishinda kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, juzi.

“Banda aliambiwa apashe, lakini akakataa kwa kuwa kocha alitaka kumuingiza,” kilieleza chanzo.

“Hali hiyo ilionyesha kumuudhi sana kocha, jambo ambalo limemfanya aiombe kamati ya nidhamu ilishughulikie,” kilifafanua zaidi chanzo.

Hivi karibuni, aliyekuwa nahodha wa Simba, Hassan Isihaka naye alimgomea Mayanja alipotaka kumpanga katika mechi ya Kombe la Shirikishi dhidi ya singida United.

Pamoja na Isihaka kugoma mbele ya wachezaji wengine, baadhi ya wachezaji hasa Hamisi Kiiza aliibuka na kumtetea kwenye mitandao jambo ambalo aliambiwa na uongozi kukanusha. Naye akafanya hivyo lakini akilaumu eti magazeti yaliandika. Lakini ukweli hakuna gazeti lililokuwa limeandika usiku huo hadi yeye alipotupia taarifa hiyo mtandaoni.

Juhudi za kumpata Mayanja na Banda bado zinaendelea na tutaapasha lolote litakaloendelea.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV