March 14, 2016

KESSY NA KIIZA...

Straika nyota wa Simba, Mganda, Hamis Kiiza, ametoa ushauri wa bure kwa viongozi wake. Amewaambia kuwa kama kuna kosa kubwa watakalolifanya ambalo litawafanya wajutie, basi ni kumuacha beki  Hassan Kessy aende Yanga.

Kiiza ambaye amewahi kuichezea Yanga, ametoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa kuwa Kessy anawaniwa na klabu hiyo.

Kessy inadaiwa hivi karibuni aligoma kusaini mkataba mpya Msimbazi, akidai dau nono la shilingi milioni 60.
 Kiiza alisema beki huyo ndiye aliyefanikisha kwa kiwango kikubwa idadi ya mabao 18 aliyofunga msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

“Kessy ni mpishi mzuri wa mabao ambaye amehusika kwa kiwango kikubwa kunitengenezea mabao mengi tofauti na wachezaji wengine kiukweli.

“Wapo wachezaji wengine walionitengenezea nafasi za kufunga, lakini kwake Kessy ni nyingi sana, amenitengenezea kwa njia ya krosi na kona anazopiga.


“Hivyo, viongozi ni vyema wakapambana vya kutosha kuhakikisha wanambakiza Kessy ili asiende huko Yanga wanaotaka kumsajili,” alisema Kiiza.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV