March 13, 2016


MPIRA UMEKWISHAA
-Mpira unaonekana kuwa taratibu sasa, Simba kiana wanapoteza muda kulinda bao lao moja
-Meshack Selemani anaingia kuchukua nafasi ya Jeremiah Juma
-Jeremiah Juma anapoteza nafasi nzuri kabisa ya kufunga baada ya mabeki wa Simba kumsahau 

DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 88, Kazimoto anawatoka mabeki wawili  wa Prisons na kupiga shuti lakini kipa anadaka kwa ulaini kabisa
GOOOOOOOO Dk 87, Awadhi Juma anapiga shuti kali kabisa nje ya 18 na kuiandikia Simba bao safi kabisa la kwanza
SUB Dk 83, Simba wanamtoa Kiiza raia wa Uganda, anaingia Kiongera Paul raia wa Kenya

Dk 75 hadi 80, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja. Hakuna timu iliyofanya shambulizi kali
Dk 74, krosi safi ya Kessy, Kapalanya anaupangua mpira na kutoka nje. Lakini sasa amelala chini pale baada ya kugongana na Awadhi Juma. Hat hivyo inaonekana Kapalata amekuwa akifanya hivyo makusudi kupoteza muda

KADI Dk 73 Asukile anamwangusha Kessy mara mbili, sasa analambwa kadi ya njano
SUB Dk 70, Simba inamtoa Majabvi na nafasi yake inachukuliwa na Awadhi Juma

Dk 67 hadi 69 mpira umesimama kwa kuwa kipa wa Prisons anatibiwa
Dk 65, Ajib anapokea pasi ya Mkude na kupiga shuti safi kabisa lakini linagonga mwamba na kurudi uwanjani
Dk 61, mkwaju safi wa Salum Kimenya unatoka juu kidogo ya lango la Simba
DK 60, Prisons wanamuingiza Fred Chudu, anatoka Kijiko
KADI Dk 59, Kessy analambwa kadi ya njano kwa kutenda madhambi

KADI Dk 56 Kipa Prisons, Beno Kapalanya analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda
Dk 51, Ajib anapiga mpira vizuri, unagonga mwamba wa Prisons na kuokolewa
Dk 46, mpira wa kichwa wa Jeremiah Juma Mgunda unagonga mwamba na kuokolewa
&&&&&&&&&

Dk -Kessy anachonga vizuri mpira wa faulo, lakini Prisons wanaondoka hatari langoni mwao
-Kessy anapata nafasi nyingine, anapiga shuti kali kabisa lakini unaishia mikononi mwa kipa
-Kiiza anapata mpira safi wa Kazimoto eneo la hatari, lakini anachelewa na Kimenya anaokoa vizuri kabisa
DAKIKA TANO ZA NYONGEZA
Dk 44, Kessy anachonga krosi nyingine ambayo inakuwa butu. Huenda hii ni krosi ya tano ya Kessy katika kipindi hiki inaonekana haina faida

Dk 43, kijiko anachonga kona nzuri ya Prisons lakini kipa Agbani anafanyiwa madhambi
Dk 41, Simba inapata kona, Kessy anaichonga vizuri lakini kipa wa Prisons anaonekana kuwa makini kabisa
Dk 38, Kipa wa Prisons yuko chini anatibiwa baada ya kugongana na Majabvi
Dk 37, Asukile anautoa mpira na kuwa kona. Inachongwa na Ajib, mpira unamfikia Kiiza, anashindwa kupiga shuti unaokolewa
Dk 30, Ajib yuko chini Ajib akitibiwa baada ya Juma Seif 'Kijiko' kumkwatua kwa makusudi kabisa ingawa mwamuzi ameonekana kulichukulia poa
Dk 29, Kessy tena, anaingia vizuri kabisa, lakini anapiga krosi ya hovyo kabisa na isiyo na msaada kwa Simba

Dk 26, Ajib anawapangua mabeki wa Prisons lakini wanawahi na kutoa, ni kona. Hata hivyo Simba haiitumii kona hiyo vizuri
Dk 21, Ajib anawachambua mabeki wawili wa Prisons na kuachia shuti kali lakini kipa anafanya kazi ya ziada na kuoa. Kona lakini haina matunda
Dk 19, Kessy tena anapoteza nafasi ya wazi baada ya Simba kugongena vizuri hadi ndani ya 18 ya Prisons lakini yeye anapaisha kabisa
Dk 17, Simba wanafanya shambulizi kali na mpira unamfikia Kessy, anapiga shuti kali vizuri kabisa lakini mpira unatoka sentimeta chache tu
Dk 15, Jeremiah Juma, anapiga mkwaju safi wa faulo lakini anapaisha juu kidogo ya lango la Simba
Dk 14, Kiiza anapoteza nafasi ya wazi kabisa baada ya kuunganisha krosi safi ya Tshabalala akiwa analitazama lango, lakini ametoa nje
KADI Dk 9, Salim Kimenya analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Ibrahim Ajib

Dk 4 hadi ya 6, inaonekana kila timu inacheza kwa hofu. Lakini Simba wanafanya mashambulizi kadhaa ambayo hata hivyo si makali yanayoweza kuitikisa ngome ya Prisons
Dk 3, Benjamini Asukile wa Prisons anamwangusha Kessy na mwamuzi anamuonyesha, kwamba wacheze mpira.

Dk ya 1, Mgosi anakuwa wa kwanza kujaribu lakini shuti lake linashindwa kulenga lango.

Kikosi kitakachoanza leo ni 
1. Vicent Angban 
2. Hassan kessy
3. Mohammed Tshabalala
4. Novatus lufunga
5. Juuko Murshid
6. Justice Majabvi 
7. Jonas Mkude
8. Mwinyi Kazimoto
9. Mussa Mgosi 
10. Ibrahim Ajib
11. Hamis Kizza

Kikosi cha akiba ni 

1. Robert Kisu 
2. Abdi Banda 
3. Awadh Juma 
4. Said Ndemla 
5. Danny Lyanga 
6. Peter Mwalyanzi

7. Said Ndemla

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic