March 6, 2016

Dakika ya 43, Mchezo umebalansi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Kipindi cha kwanza kimemalizika, timu zote zimeingia vyumbani kwa ajili ya mapumziko ya dakika 15.


Kikosi cha Simba:
1. Vincent Angban
2. Emiry Nimubona
3. Mohamed Hussein ‘Tshabalala’
4. Novaty Lufunga
5. Juuko Murshid
6. Justice Majabvi
7. Mwinyi Kazimoto
8. Jonas Mkude
9. Hamis Kiiza
10. Ibrahim Ajib
11. Brian Majwega

Kikosi cha Mbeya City


1. Hannington Kalyesebula
2. Hassan Mwasapili
3. Abubakar Shaban
4. Tumba Sued
5. Haruna Shamte
6. Kenny Ally
7. Raphael Alpha
8. Haruna Moshi ‘Boban’
9. Geofrey Mlawa
10. Joseph Mahundi
11. Ditram Nchimbi

Haruna Moshi ‘Boban’ wa Mbeya City alipata kadi ya njano katika dakika ya 45 kabla ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mapumziko.


Kumbuka kuwa mpaka sasa Simba inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi kuu Bara ikiwa na pointi 45, wakati Mbeya City inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 21.

Simba ikishinda itaongoza ligi kwa kuwa na pointi 48 katika michezo 21, wakati Mbeya City ikishinda itafikisha pointi 24 hivyo kupanda hadi nafasi ya tisa katika michezo 21.

Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza.

Simba wamefanya mabadiliko, ametoka Majwega ameingia Danny Lyanga

Matokeo bado ni 0-0 

Dakika ya 57: Simba wameotea mara 9, Mbeya City wameotea mara 1

Dakika ya  58: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Hamis Kiiza anaingia Awadhi Juma.

Dakika ya 62: Shuti kali la Jona s Mkude linatoka pembeni kidogo ya lango la Mbeya City.

Dakika ya 67: Mbeya City wanafanya mabadiliko, anatokaBoban anaingia Themi Felix.

Dakika ya 68: Simba wanafanya mabadiliko mengine, anatoka Nimubona anaingia Hassan Kessy.

Mchezo ni mkali na kuna mashambulizi ya zamu, mchezo bado ni 0-0.

Dakika ya 75: GOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!! 
 
Mfungaji wa bao la Simba, Danny Lyanga


 Simba imepata bao dakika ya 75 likifungwa na Danny Lyanga. Kiungo Ibrahim Ajib alifanya kazi nzuri ya kuwatoka mabeki wa Mbeya City, akampa pasi, Awadhi Juma ambaye alipiga shuti kali lililopanguliwa na kipa wa Mbeya City, kisha Lyanga ambaye alikuwa karibu, akautupia mpira wavuni.

Dakika ya 77: Mchezo umechangamka zaidi.
 
Dakika ya 79: Kenny Ally wa Mbeya City anapata kadi ya njano kwa kumkwatua Jonas Mkude.

Dakika ya 90; Ibrahim Ajib anafunga bao kali dakika ya 90, Simba 2, Mbeya City hawajapata kitu.

Ajib aliwakokota mabeki wa Mbeya City upande wa kushoto kisha akapiga mpira ambao uliwababatiza mabeki hao na kipa wao, kisha kujaa wavuni moja kwa moja.

Ajib anashangilia kwa kwenda ndani ya wavu wa lango la Mbeya City huku akipongezwa na wenzake.

Ibrahim Ajib

MPIRA UMEMALIZIKA: Simba 2-0 Mbeya City  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic