March 6, 2016



 Mabao mawili yaliyofungwa na Danny Lyanga na Ibrahim Ajib katika dakika ya 75 na 90 yameipa Simba ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Danny Lyanga
 Simba imepata ushindi katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambapo sasa imeshika usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 48 ikiizidi Yanga ambayo ina pointi 47 sawa na Azam inayoshika nafasi ya tatu.

Ushindi huo ulisababisha shangwe nyingi kwa mashabiki wa Simba ambao waliondoka uwanjani hapo wakiwa na furaha huku wakishangilia barabarani.

Mara baada ya mchezo huo, Kocha wa Simba, Jackson Mayanja alisema anashukuru mashabiki wa timu yake kwa kuendelea kuiunga mkono timu yao huku akipongeza wachezaji wake kwa kuifunga Mbeya City kwa mara ya kwanza katika uwanja huo.

Upande wa Mbeya Ciy, Kinnah Phiri alisema kilichotokea ni timu yake kukosa bahati tu lakini vijana wake walicheza vizuri. Kingine alisema wachezaji wake walikuwa wakipata nafasi ya kupiga mashuti lakini hawakufanya hivyo, ameahidi kwenda kulifanyia kazi suala hilo.

 Simba ilivyotoa nishai Mbeya City...

Mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza akidhibitiwa na mabeki wa Mbeya City.

 
Ibrahim Ajib wa Simba (kushoto) akijiandaa kumtoka beki wa Mbeya City, Haruna Shamte huku kwa mbalii Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri akishuhudia purukushani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic