Kama huwa unashangaa yale mambo ya Yanga na Simba kwa mashabiki wa upande mmoja kuunga mkono timu za wageni, chukua hii hapa kutoka Rwanda.
Katika mazoezi yake kwenye Uwanja wa Ferwafa eneo la Remara jijini Kigali, mashabiki wa Rayon Sports ambao ni wapinzani wakubwa wa APR walijitokeza mazoezini na kuiunga mkono Yanga kwa nyimbo na machombezo.
Yanga ipo Kigali, Rwanda kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR. Itapigwa kwenye Uwanja wa Amahoro, kesho.
Pamoja na kuwa ugenini, Yanga wala haina shida ya mashabiki kwa kuwa tayari mashabiki wa Rayon Sports wameishajitokeza kuiunga mkono kwa nguvu.
Katika mazoezi yake kwenye Uwanja wa Ferwafa eneo la Remara jijini Kigali, mashabiki wa Rayon Sports ambao ni wapinzani wakubwa wa APR walijitokeza mazoezini na kuiunga mkono Yanga kwa nyimbo na machombezo.
Hali ambayo inaonyesha, kesho watakuwa uwanjani kuendelea kuiunga mkono kwa nguvu zote.
APR na Rayon zina upinzani mkubwa katika soka nchini Rwanda kama ilivyo kwa Yanga na Simba nchini Tanzania. Hivyo mashabiki wa Rayon wanataka kuona APR ikiadhibiwa na Yanga hiyo kesho.
0 COMMENTS:
Post a Comment