May 5, 2021


 SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeongeza idadi ya wachezaji wa akiba kutoka 7 hadi 9 kuanzia hatua ya Robo Fainali itakayochezwa tarehe 14 Mei, 2021.


Aidha kuhusiana na idadi ya wachezaji watakaoingia kwenye mechi moja CAF wanasema vilabu vitataarifiwa hivi karibuni baada ya marekebisho yanayotarajiwa kufanywa na FIFA kupitia IFAB (International Football Association Board) ambao wanahusika na marekebisho ya sheria na kanuni.

Habari hiyo itakuwa njema kwa timu ambazo zinashiriki  Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwa Tanzania, Simba wapo hatua hiyo wakiwa wananolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes. 

Pia Mashirikisho/Vyama vya Soka vimetaarifiwa kuviambia vilabu vitakavyoshiriki Mashindano yajayo ya CAF (Inter club Competitions) kwa msimu wa 2021/2022 kuwa wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa Kamati ya Mashindano ya CAF kupitia CMS (Competition Management System) sio zaidi ya tarehe 30 Juni, 2021.

Taarifa hiyo ilitolewa na Caf, Mei 3, 2021 kwa ajili ya nchi zote za Afrika ambazo zinashiriki mashindano ambayo yanaandaliwa na Caf.



6 COMMENTS:

  1. Ndiyo maana tukasema this is Bonanza Tournament,.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna akili brother,huwezi kukashifu taarifa za watu ikiwa wewe huwezi hata kutoa mchango wa mawazo,mpira umejengewa mifumo na wanadamu hivyo waowao wanao uwezo wakuboresha pale wanapoona hapako Sawa,sasa unaposema this is bonanza tonament unamaanisha nn ikiwa hawa wanaorekebisha ndio walio simika kanuni hizo,jitahid kua na stara mpendwa.

      Delete
    2. Eti Bonanza.... Mawazo ya waliofeli utayajua tu. Akili zao zipo kiuto uto

      Delete
  2. Mawazo ya kifukara.UEFA champions league nao walio benchi ni 9 nao ni bonanza.Ukiwa umefeli kwenye maisha au mafanikio unakuwa na roho ya husda na kinyongo ukitaka wote wawe kama wewe.Kufeli na kukosa maendeleo ni ugonjwa mbaya sana.

    ReplyDelete
  3. Kama ni bonanza yeye Yuko nafasi ipi kwenye mashindano ya ndani na nje

    ReplyDelete
  4. Unazungumzia Mikia Mazuri tu Yanga unaiponda tu.

    Ulivyo mwandishi uchwala

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic