March 16, 2016


TANZANIA PRISONS

Tofauti na wengi wanavyodhani kuwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu unawaniwa na timu tatu pekee; Simba, Yanga na Azam lakini kumbe Tanzania Prisons maarufu kama "Wajelajela", nao wapo makini katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zao zilizobaki ili wachukue taji hilo.

Nahodha wa Prisons, Laurian Mpalile, ameeleza wazi mapambano yao, akibainisha kuwa nafasi bado wanayo na wamedhamiria kuhakikisha hilo linatimia, hivyo wanaendelea kupambana katika michezo yao iliyobaki.

“Nafasi bado tunayo, hatupo sehemu mbaya, naweza kusema hatujakata tamaa ya ubingwa na tunapambana katika hilo, nia yetu sasa ni kushinda katika michezo iliyobaki na kupata matokeo mazuri zaidi, ndiyo maana hata kwenye mechi yetu na Simba tulijitahidi katika hilo lakini tukapoteza mchezo dakika za mwisho,” alisema Mpalile.


Prisons kwa sasa inashikilia nafasi ya tano ikiwa na pointi 36 baada ya mechi zake 23, ikiwa imepishana kwa jumla ya pointi 18 na vinara Simba waliocheza mechi 23 na kukusanya pointi 54. Prisons imebakisha michezo saba, kama itashinda yote itakusanya pointi 21 jumla, lakini itaiombea Simba ipoteze mechi zake zote zilizobaki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV