March 9, 2016

HALL NA PLUIJM
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amemvaa kocha msaidizi wa Azam FC, Dennis Kitambi kwa kumtaka akaurudie upya kuutazama mchezo wao ili kuona usahihi wa mwamuzi kufuatia madai ya mwamuzi kukataa penalti baada ya Kelvin Yondani kuushika mpira kwa mkono katika eneo la hatari baada ya kudondoka.

Azam na Yanga zilitoka sare ya mabao 2-2, Jumamosi iliyopita katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo uliokuwa na malalamiko kufuatia Azam kutoa madai ya kuhujumiwa.

Aidha, katika mchezo huo mwamuzi Kennedy Mapunda, alikataa bao la Azam, ambapo beki Shomari Kapombe alifunga katika kipindi cha kwanza  kwa madai kuwa mfungaji alikuwa ameotea.

Pluijm alimtaka Kitambi kwenda kuangalia mechi hiyo kwa mara ya pili kupitia CD na si kulalamika kuwa wamekoseshwa penalti na kudai kuwa Yondani alisukumwa na John Bocco kwa mikono miwili.

“Usilalamike kuwa mwamuzi hakuchezesha vizuri mchezo, kwa upande wangu waamuzi naona wako sahihi na ile haikuwa penalti kwani Yondani alisukumwa kwa mikono miwili ndiyo maana alianguka chini na kutokea tukio lile.

“Ni vyema kwenda kuuangalia mchezo huu kupitia CD kisha utaona kilichotokea na si kumlalamikia mwamuzi, kwa upande wangu sikufurahishwa na matokeo haya kwani lengo langu lilikuwa ni kushinda kwani hakukuwa na sababu ya kutoa sare.


“Nitajipanga kwa ajili ya michezo ijayo ili kuweza kufanya vyema,” alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic