March 11, 2016


Uongozi wa Yanga umeanza mipango ya kusaini mkataba mpya na beki wao wa kati, Kelvin Yondani lakini licha ya kukabidhiwa mkataba mpya, mpaka sasa mchezaji huyo hajasaini wala kufanya mazungumzo zaidi.

Yondani ambaye alitua Yanga msimu wa 2010/2011 akitokea Simba, aliliambia gazeti maarufu la michezo nchini la Championi kwamba hatasaini mkataba mpya ikiwa hatapatiwa shilingi milioni 60 kama ada ya usajili.

Lakini taarifa ilizozipata SALEHJEMBE kutoka ndani ya Kamati ya Utendaji ya timu hiyo, zinasema uongozi wa Yanga umeshampatia mkataba huo lakini bado mazungumzo hayajafanyika.

“Wachezaji wote muhimu ambao kocha ameomba waongezewe mikataba ambayo inamalizika mwishoni mwa msimu huu, tupo kwenye mazungumzo nao.

“Kati ya wachezaji hao yumo Yondani ambaye ni beki wa kutegemewa kwenye timu ambaye yeye tayari tumempa mkataba,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit kuzungumzia hilo, alisema: “Wachezaji wetu wote ambao mikataba yao imemalizika tupo kwenye mazungumzo nao kwa ajili ya kuwaongezea akiwemo huyo Yondani.


“Pia uongozi upo kwenye mazungumzo na makocha wetu Pluijm (Hans) na Pondamali (Juma) ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu.” 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic