March 11, 2016


Anabaki au anaondoka! Maajaaliwa ya beki wa pembeni wa Simba, Hassan Kessy, bado hayajajulikana ambapo haijajulikana ataendela kuichezea Simba au ataondoka kutokana na mabosi wake kutofautiana juu yake.

Kessy anaelekea mwisho wa mkataba wake ambapo amesaliwa na miezi miwili tu, ambapo kwa mujibu wa kanuni za usajili anaruhusiwa kuzungumza na klabu nyingine yoyote juu ya usajili lakini upande wa Simba wameonyesha kama sitaki nataka.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza  mabosi wamegawanyika makundi mawili, wapo wanaomtaka na wasiomtaka Kessy aongeze mkataba mpya wa kuichezea Simba.

“Hadi muda huu ninaoongea na wewe, kuna makundi mawili; wanaomkubali na wanaotaka aondoke, kuna kiongozi mmoja mkubwa yeye tayari ameanza mazungumzo na meneja wake Tippo (Athumani) kwa ajili ya kumuongezea mkataba, pia yupo mjumbe mmoja kutoka kwenye Kamati ya Usajili ambaye hamtaki Kessy,” alisema mtoa taarifa wetu.


Alipotafutwa meneja wa mchezaji huyo, Tippo alisema: “Bado hatujaanza mazungumzo rasmi na viongozi wa Simba, lakini kama wakija tutazungumza nao, pia nimepokea ofa kwenye baadhi ya klabu zikimhitaji Kessy.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic