Bao la Angelo Correa limeifanya Atletico Madrid iendelee kuwa
kwenye ramani ya ushinda wa La Liga.
Bao hilo pekee katika dakika ya 63, limeipa Atletico ushindi wa
bao 1-0, sasa inaendelea kubaki katika nafasi ya pili kwa msimamo wa La Liga.
Ilikuwa mechi kali na licha ya kuwa ugenini, Atletico ilionyesha
imepania kushinda.
Kocha wake, Diego Simeone alikuwa jukwaani akitumikia adhabu
lakini midadi yake ilikuwa kama kawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment