April 19, 2016

MCHEZO UMEMALIZIKA 
 
ESPÉRANCE DE TUNIS 3-0 AZAM FC

Dakika 94+ zimekamilika, Azam wanafungwa mabao 3-0 na hivyo kutolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa jumla ya mabao 4-2.

Dakika ya 93+

Dakika nne za nyongeza, mwamuzi wa akiba ameonyesha dakika nne za nyongeza.

Dakika ya 90: Mashabiki wa Esperance wanafanya fujo, wanatibuana na polisi lakini mchezo unaendelea.

Dakika ya 88: Wachezaji wa Azam wanaonekana kukata tamaa.

Dakika ya 85: Azam wapo nyuma kwa mabao 3-0.

Bao la tatu lilifungwa na Ben Yousef

Esperance wanapata bao la tatu kutokana na kupigiana pasi vizuri na kuwaacha mabeki wa Azam wakiwa hawajui cha kufanya.

Anatoka Waziri Salum anaingia Didier Kavumbagu

Dakika ya 79: Azam wanafanya mabadiliko, anatoka Sure Boy anaingia Himidi Mao.

Dakika ya 73, Azam wanapambana kutafuta bao.

Dakika ya 71, Azam wanafanya mashambulizi kupitia kwa Singano lakini shuti lake linaishia mikononi mwa kipa wa Esperance.


Azam wanafanya mabadiliko, anatoka Farid Mussa anaingia Khamis Mcha.


Mfungaji wa bao la pili ni Haythem Jouini.
 

Dakika 62: Azam wapo nyuma kwa mabao 2-0.

Dakika ya 60: Esperance wanakosa bao kutokana na kona iliyopigwa langoni mwao.

Dakika ya 59: John Bocco anachechemea huku mchezo ukiendelea.

Dakika ya 58: Esperance wanapata kona.

Dakika ya 50: Esperance bado wanalishambulia lango la Azam.

Dakika ya 46: Singano anapata kadi ya njano kutokana na kwenda kulalamika kwa mwamuzi baada ya bao hilo kuingia.

Mfungaji wa bao hilo ni Saad Bguir

Dakika ya 46: Esperance wanapata bao.

GOOOOOOOOOOO!!!!!!!!

Kipindi cha pili kimeanza.

Dakika 45 zimekamilika, mchezo ni mapumziko, matokeo bado 0-0.

Dakika ya 45: Esperance wanapata kona, wnafanya shambulizi kali, wanapiga Aishi anaokoa, inakuwa kona tena, inapigwa lakini Azam wanaokoa inakuwa goal kick.


Dakika ya 44: Gooooo!!! NOOOOOO!!!! Esperance wanatupia mpira wavuni lakini mwamuzi anakataa na kusema mfungaji alikuwa ameotea.

Dakika ya 43: Farid Musa akishirikiana na John Bocco wanafanya shambulizi kali lakini Esperance wanaokoa.

Dakika ya 42: Waziri Salum anapata kadi ya njano kutokana na kucheza faulo.

Dakika ya 40: Esperance wanafanya shambulizi kali lakini Aishi anaokoa.

Mashabiki wa Esperance wanashangilia muda wote, licha ya baridi wao wanaendelea kushangilia baadhi yao wakiwa vifua wazi.
 


Dakika ya 40: Esperance wanapata kona lakini inaokolewa.

 Dakika ya 38: Beki wa Azam FC, Waziri Salum yupo chini, mchezo umesimama kutokana na kuwa aliumia.

Dakika ya 36: Esperance wanafanya shambulizi kali, mpira ulimpita Aishi ukawa unaelekea langoni, lakini Aggrey Morris akauwahi na kuokoa mpira ukiwa unaelekea langoni.

Dakika ya 32: Shuti kali langoni kwa Azam lakini Aishi anafanya kazi nzuri kuokoa.


Dakika ya 30: Espérance wanafanya mashambulizi ya nguvu, Azam wanahitaji kuwa makini zaidi.

Dakika ya 27: Esperance wanafanya shambulizi kali, mpira unagonga mwamba. Mashabiki wa Espérance walikuwa wameshanyanyuka kushangilia.

Dakika ya 23: Singano na Azam anaingia na mpira katika eneo la 10 la Esperance na lakini kipa anauwahi mpira na kuudaka.

Dakika ya 21: Wenyeji wanafanya mashambulizi lakini walinzi wa Azam wanakuwa makini, Singano anarejea nyuma kusaidia kukaba. Hali ya hewa ni baridi kiasi.

Dakika ya 17: Singano anaisumbua safu ya ulinzi ya Esperanse lakini wenyeji wanajibu mashambulizi kwa kufanya shambulizi kali, kipa wa Azam Aish Manula anaokoa.

Wenyeji wanaonekana wakicheza staili ya offside trick, wachezaji wa Azam wanajikuta wakiotea mara kwa mara.


Dakika ya 14: Esperance wanapata kona lakini Azam wanaokoa.

Dakika ya 12: Ramadhani Singano anakimbilia mpira lakini anakuwa offside.

Dakika ya 10: Matokeo bado ni 0-0, Azam FC wanaonekana kutulia.

Dakika ya 6: Esperance wanaonekana kuanza kuchangamka kwa kucheza mpira wa kasi.

Dakika ya 4: Azam FC bado wanaonekana kutulia.

Dakika ya 2: Mchezo bado haujashika kasi.

Mchezo umeanza.

Kikosi cha Azam FC ambacho kitaanza pamoja na wale wachezaji wa akiba tayari wameshaingia uwanjani kupasha misuli.




Kikosi cha Azam FC kitakachoanza leo dhidi ya Esperance ya Tunisia kwenye Uwanja wa Olympique de Rades katika mechi ya Kombe la Shirikisho. Mchezo unatarajiwa kuanza saa 3.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki:
 

28 Aishi Salum
6 Erasto Nyoni
26 Wazir Salum
12 David Mwantika
13 Aggrey Morris
29 Michael Bolou
14 Ramadhan Singano
18 Frank Domayo
8 Salum Abubakar
19 John Bocco (C)
17 Farid Mussa

AKIBA
1 Mwadini Ali
15 Said Morad
23 Himid Mao
22 Khamis Mcha
20 Mudathir Yahya
9 Allan Wanga
11Didier Kavumbagu

2 COMMENTS:

  1. MUNGU IBARIKI AZAM,MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  2. Kama hawa walifungwa 2-1 mechi ya kwanza leo wameshinda 3-0,je wale waliotoka sare ya 1-1 mechi ya kwanza leo si itakuwa balaa!?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic