April 19, 2016


YANGA WAKIWA NCHINI MISRI

YANGA WAKIWA NCHINI MISRI


Mshambuliaji wa Yanga, Amiss Tambwe amesema kuwa kila kitu kinaenda vizuri katika maandalizi yao kuelekea mchezo dhidi ya Al Ahly, kesho Jumatano.

Yanga ipo jijini Alexandria nchini Misri kukipiga dhidi ya wenyeji wao hao katika mechi ya pili ya Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo katika mchezo wa awali timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Akizungumza na salehjembe, Tambwe ambaye yupo pamoja na kikosi cha Yanga jijini Alexandria, amesema kuwa upande wake yeye hajaona figisu zozote mpaka sasa na morali ya wachezaji wote inaonekana ipo juu, hivyo anaamini watafanya vizuri katika mchezo huo.

TAMBWE KATIKA MECHI YA KWANZA ILIYOCHEZWA DAR ES SALAAM

“Tupo vizuri, ndiyo tumetoka mazoezini muda si mrefu, binafsi sijaona jambo lolote baya naamini tutafanya vizuri, tumuombe Mungu kila kitu kiende salama kama ilivyo sasa,” alisema Tambwe.

Yanga inahitaji ushindi wowote katika mchezo huo au sare ya zaidi ya bao moja, ikifanikiwa hivyo itasonga katika hatua ya makundi kuungana wakati ikitolewa itashushwa mpaka kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo huko itacheza atua ya mtoano na timu itakayofanya vizuri itafuzu hatua ya makundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV