April 19, 2016


 Leo nilifanya ziara fupi kwenye Uwanja wa Raizor unaomilikiwa na klabu ya Derpotivo la Coruna nikiongozana na washindi wa “Kwea Pipa Kwenda Spain na Azam Sports HD Sports”.

Tulipita katika sehemu mbalimbali za uwanja huo, mimi na washindi hao kutoka Yanzania pamoja na washindi wengine wanne kutoka Sweden na Hong Kong pamoja na wenyeji wetu tulijifunza mengi.

Lakini kilichonifurahisha ni kuona maandalizi ya sehemu ya kuchezea, yaani pitch ikiwa katika maandalizi makubwa.

Nilitaka kujua ni katika mechi dhidi ya Barcelona tu kwa kuwa ni kubwa. Jibu lilikuwa hapana na maandalizi huwa kila mara lakinim kabla ya mechi, lazima kuwe na maandalizi kama hayo.

Kesho kwenye uwanja huo Barcelona watakuwa wageni dhidi ya Derpotivo ambayo nayo haina mwendo mzuri.

Nikukumbushe tu kwamba mechi hiyo itaonyeshwa kesho moja kwa moja kupitia Azam Sports HD kwenye king'amuzi cha Azam. Wakati unacheki mechi, angalia uwanja utakavyokuwa smart, halafu utupie maoni yako hapa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV