April 19, 2016

Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas ametaja kikosi cha wachezaji 11 ambacho anaamini kuwa ni bora kwake katika Premier League ndani ya msimu huu wa 2015/2016 lakini hakuna jina hata moja la mchezaji kutoka Chelsea.


Katika kikosi hicho cha kiungo huyo kuna wachezaji wengi kutoka Leicester City na Tottenham, timu mbili ambazo zipo kwenye mbio za ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Fabregas alisema hayo alipokuwa mgeni katika kipindi cha Monday Night Football katika kituo cha runinga cha Sky Sports.

Licha ya kukiri kuwa kiungo mwenzake wa Chelsea, William amekuwa akicheza vizuri msimu huu lakini hakumtaja katika wale 11 bora.“Siyo kazi rahisi kuchagua hasa katika safu ya mlinda mlango, Kasper Schmeichel amefanya kazi nzuri na anastahili kuwemo katika kikosi hiki lakini De Gea ameokoa pointi nyingi za Man Utd. Mungu mwenyewe anajua ni pointi ngapi,” alisema Fabregas.

Kikosi kizima cha Fabregas kinasomeka hivi:


1. David de Gea
2. Hector Bellerin
3. Toby Alderweireld
4. Robert Huth
5. Ryan Bertrand
6. Riyad Mahrez
7. N'Golo Kante
8. Dele Alli
9. Dimitri Payet
10. Jamie Vardy
11. Harry Kane 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV