April 2, 2016
Kipindi cha pili, mwanzoni kilionekana kuwa cha Barcelona, lakini kadiri muda unavyosonga mbele, mambo yalibadilika.

Madrid imepata bao mwishoni kupitia Cristiano Ronaldo, hata hivyo ilikuwa ni dakika chache baada ya kupoteza nafasi nyingine mbili kupitia Bale.

Kuanzia dakika ya 75, Barcelona walionekana kupoteza hali ya makini na kuruhusu Madrid kupitia kulia kutoka upande wa Alba ambaye alionekana kupwaya, kuingia katikati na kusababisha madhara mengi zaidi.


Mapumziko:
Mechi ya wababe wa soka barani Ulaya, Barcelona dhidi ya wageni wake Real Madrid ni ngumu. Sasa ni mapumziko na hakuna timu iliyopata bao.

Lakini kumekuwa na kosakosa kila upande na mechi inaonekana kutokuwa na mwenyewe.

Inawezekana kabisa Barcelona wanapaswa kubadilika zaidi katika kipindi cha pili na kurudi katika mchezo wao.


Inaonekana kama Real Madrid wameweza kuwabana na kuwaalazimisha wacheze wanavyotaka huku wao Madrid wakipoteza nafasi tatu za kufunga kupitia Karim Benzema mara mbili na Gareth Bale mara moja.

Barcelona pia mara mbili imejaribu kupitia Raktic ambaye anaonekana kuwa katika kiwango kizuri leo.

Kila upande zimetolewa kadi mbili za njano, Barcelona ni Luis Suarez na Javier Mascherano na Madrid ni Sergio Ramos na Daniel Carvajal. Huenda ni dalili za kadi nyekundu pia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV