April 2, 2016


Yanga imeambiwa iache kulalamika kuhusu mabadiliko ya ratiba ya mechi za Ligi Kuu Bara na badala yake inatakiwa kucheza soka uwanjani.

Awali, Simba ililalamika yenyewe kutangulia kwa mechi 24 huku Yanga na Azam FC zikiwa na michezo 21 tu na mechi zao zikiahirishwa ili washiriki mechi za kimataifa za Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Baada ya Simba kutishia kususia mechi za ligi hadi ifanane idadi ya michezo na timu hizo, Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) ikabadilisha ratiba ambapo Yanga na Azam zitalazimika kucheza mechi mbili kwa wiki.

Kutokana na hali hiyo, Yanga na Azam tayari zimelalamika kuhusu ratiba hiyo lakini, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe amewaambia: “Tulieni, acheni maneno chezeni mpira.”

Hans Poppe amesema kuwa Yanga na Azam hazina sababu ya kulalamika kwa kuwa hayo mambo waliyataka wenyewe huku wakifurahia kutocheza michezo hiyo awali na sasa inawabana hivyo wanapaswa kukubaliana na matokeo.

“Nashangaa Yanga wanalalamika nini kupewa ratiba mpya, hiyo ilifahamika kwamba mwisho wake utakuwa huu, lazima ligi iishe kwa siku moja sasa wao kwa viporo vyao walifikiri watamaliza lini? 


“Yanga waache maneno yao, si wamesajili wachezaji zaidi ya 25? Wachezea mpira, kwanza wanacheza kila baada ya saa 72 kama inavyosema kanuni, hapo hakuna tatizo.”

2 COMMENTS:

  1. Huyo mtuhumiwa wa uhaini akili zake bado kutulia toka aachiwe kutoka keko,kati ya simba na yanga ni akina nani wamepeleka malalamiko hadi kwa waziri?
    Kwahiyo nawe mshika kalamu unatakiwa kuintagret kauli za watu kabla ya kuhabarisha hadhira!

    ReplyDelete
  2. Mtanyamaza tu nyie wa mchangani,na tumewazoea na maneno yenu maana kwenu msemaji wa club hajulikani wote ni waongeaji,Na ubingwa hamuupati ng'o.Kuna mtu alikuwa anaongea kama Rage?yuko wapi sasa?Igeni basi tabia za kimataifa maana YANGA NI KIMYAKIMYA TU TUNASEMA INAPOBIDI.GOD BLESS YANGA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic