April 2, 2016



Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, jana Ijumaa alikutana na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wale wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzungumza namna ya kuweka mambo sawa juu ya deni linaloikabili TFF.

Juzi Alhamisi, TRA ilikamata magari matano ya TFF kutokana na kulidai shirikisho hilo Sh bilioni 1. 118 ikiwa ni malimbikizo ya madeni ya kodi kuanzia mwaka 2009.


Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, ameliambia Championi Jumamosi kuwa: “Tunashukuru Waziri Nape kwa kufanya jambo kama hili kwani tulikuwa na mazungumzo mazuri, wenzetu wa TRA wametoa ushirikiano mzuri na mambo yataenda sawa.”

Hata hivyo, TFF imekuwa ikisisitiza kuhusiana na deni hilo kwamba kama ni makato ya kodi ya serikali kutoka kwenye mishahara (PAYE) ya makocha wa kigeni, wao hawahusiki.

TFF wamekuwa wakisisitiza kwamba PAYE ya makocha hao inapaswa kulipwa na serikali kupitia wizara ya fedha na si wao.

Bado TRA haijawahi kutoa ufafanuzi kupitia suala hilo kwamba usahihi ni upi lakini imekuwa ikiendelea kulisisitiza deni hilo bila ya utani hata kidogo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic