April 21, 2016

Straika wa Leicester City, Jamie Vardy anatarajiwa kuikosa mechi dhidi ya Manchester United kutokana na kukubali kupokea adhabu baada ya kupewa kadi nyekundu kwa kumbugudhi mwamuzi wakati wa mechi dhidi ya West Ham United.Chama cha Soka cha England (FA) kilisema kitamwongeza adhabu mchezaji huyo kwa tukio lake hilo la kumsumbua mwamuzi Jon Moss baada ya kupewa kadi nyekundu kwa kujirusha ndani ya eneo la 18 la West Ham, lakini FA ilitoa muda mpaka jana jioni kuwa anaweza kukata rufaa.

Taarifa iliyotolewa jana jioni ilieleza kuwa Vardy amekubali kosa na yupo tayari kwa adhabu.

Ikiwa atapewa adhabu anaweza kuikosa mechi dhidi ya Swansea City, wikiendi hii pamoja na ile inayofuata dhidi ya Manchester United mnamo Mei 1, 2016.

Kukosekana kwa straika huyo kunaweza kuathiri katika mbio za ubingwa wa Premier League kwa timu yake inayoshika usukani wa ligi ikiwa pointi tano mbele ya Tottenham.MECHI ZA LEICESTER CITY ZILIZOSALIA
April 24 Swansea City (nyumbani)
May 1 Manchester United (ugenini)
May 7 Everton (nyumbani)
May 15 Chelsea (ugenini)


MECHI ZA TOTTENHAM ZILIZOSALIA
April 25 West Bromwich Albion (nyumbani)
May 2 Chelsea (ugenini)
May 8 Southampton (nyumbani)
May 15 Newcastle United (ugenini)

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV