April 21, 2016

Licha ya kuonyesha uwezo mzuri kwa kutoa asisti nyingi na kufunga mabao katika Premier League msimu huu, kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil hayumo katoka orodha ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha msimu katika ligi hiyo maarufu kwa jina la PFA Team of the Year.


Kikosi hicho ambacho kimetajwa na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) hakijataja jina la Ozil kama wengi alivyokuwa wakimtegemea huku chipukizi wengine wakitajwa kuwa ndiyo wanaounda kikosi hicho.

Baadhi ya chipukizi waliotajwa katika safu ya kiungo ya kikosi hico ni Dimitri Payet, N'Golo Kante, Dele Alli na Riyad Mahrez.
Mpaka sasa kabla ya mechi ya leo usiku, Ozil ametoa asisti 18 na kufunga mabao 6 na amekuwa katika kikosi cha kwanza kwa muda wote msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV