April 21, 2016

Baadhi ya mashabiki wa Liverpool wamekasirishwa na kitendo cha klabu hiyo kumchagua mshambuliaji wao wa zamani, Michael Owen kuwa balozi wa klabu katika masuala ya kimataifa.

Mashabiki hao wanadai kuwa siyo sawa kwa Owen kuwa balozi wao wakati aliwahi kuhamia katika timu ambayo ni wapinzani wao wakubwa, Manchester United.Owen aliifungia Liverpool mabao 158 katika mechi 297 alizocheza kikosini hapo akitokea kwenye kituo cha kukuzia vipaji kinachomilikiwa na Liverpool, lakini baadaye alihama na kwenda Real Madrid, hakufanikiwa sana ndiyo akarejea England na moja ya klabu aliyoichezea ni hiyo ya United maarufu kwa jina la Mashetani Wekundu.

Katika ubalozi wake huo atakuwa akizunguka katika mataifa mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza Liverpool, lakini maoni yaliyotolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo ya mitandao ya jamii inaeleza kuwa ni msaliti.

“Nani balozi! Michael Owen? Hapana kwa kweli bora nimchague El Hadji Diouf kuliko Owen,” alisema shabiki mmoja.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV