April 10, 2016


Ukisema huu ni wakati wa Anthony Joshua hautakuwa umekosea. Kwa sasa bondia huyo mcheshi lakini mwenye makonde hatari yuko on fire.

Joshua amefanikiwa kumaliza ubishi kwenye pambano lililochezwa kwenye Ukumbi wa O2 Arena nchini England kwa kumtwanga Mmarekani Prince Charles Martin kwa KO katika raundi ya pili baada ya kumwangusha mara mbili.

Prince alikuwa akiaminika bondia mwenye mkono hatari wa kushoto katika uzito wa juu kwa sasa. Lakini leo alionekana hana makali kutokana na makonde mazito ya Joshua ambaye hilo lilikuwa ni pambano lake la 16 na yote 16 ameshinda kwa KO.

Ushindi huo unamfanya Joshua kuingia kwenye rekodi ya Mwingereza wa pili kubeba mataji makubwa ya uzito wa juu, wa kwanza akiwa ni Lenox Lewis.AKISHANGILIA NA BABA YAKE

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV