April 10, 2016

 Manny Pacquiao amemaliza ubishi kwa kumtwanga bondia Mmarekani, Timothy Bradley kwa pointi.

Katika pambano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi maarufu wa MGM Grand jijini Las Vegas, Marekani, Pac alimwangusha Bradley mara mbili katika raundi ya saba na tisa na mwisho majaji wote watatu wakampa ushindi wa pointi.

Pacquiao ndiye alitawala zaidi akifikisha makonde 122 kwenye mwili wa mpinzani wake katika 439 wakati Bradley alifikisha ngumi 99 kati ya 302 alizorusha.

Wakati wanakutana, kabla ya kupanda ulingoni rekodi zao zilikuwa zinaonyesha Pacquiao (58-6-2)  na Bradley (33-2-1).
3 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV