April 3, 2016

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI

Kamati ya nidhamu ya TFF, jana ilikaa na kuhitimisha kila kitu kuhusiana na sakata la upangaji matokeo katika mechi mbili za mwisho za Ligi Daraja la Kwanza.

Geita Gold Mine ilishinda kwa mabao 8-0 dhidi ya JKT Kanembwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini  Kigoma huku Polisi Tabora ikiitwanga 7-0 JKT Oljoro ikiwa mjini Tabora.

Hapo ndipo zikaibuka tuhuma za rushwa ambazo jana zimetolewa hukumu na leo kutangazwa rasmi. Kipa wa zamani wa Simba B, Denis Richard ambaye alitua Geita Gold Mine, naye amekutana na apanga la kufungiwa miaka 10 akihusishwa na upangaji matokeo.

WALIOKUTWA NA RUNGU NA WALIOSALIMIKA:
1. Refa wa mchezo Kanembwa na Geita Akafungiwa maisha kujihusisha na mpira
2.Kamisaa wa mchezo huo naye akafungiwa maisha
3. Kocha Msaidizi wa Geita, Choke Abeid naye kafungiwa maisha 4. Kipa JKT Oljoro, Mohammed Mohammed kafungiwa miaka 10 na faini milioni 10 (alikiri kuahidiwa fedha).
5Kipa Geita, Denis Richard anafungiwa miaka 10 faini milioni 10
6.Katibu wa Chama cha mpira Tabora kafungiwa maisha.

7. Refa Masoud Mkeremi kati ya Polisi na Oljoro kafungiwa miaka 10 faini milioni 10
8. Kocha msaidizi Polisi Tabora kafungiwa maisha
9. Mwenyekiti Oljoro kafungiwa maisha.
10. Mwenyekiti wa Chama cha mpira Tabora, Yusuf Kitumbo kafungiwa maisha!
11. Geita na Kanembwa zimeshushwa Daraja. Kanembwa Ligi ya Mkoa Geita Daraja la pili
12. Polisi Tabora na Oljoro zimeshushwa Daraja hadi Daraja la pili.

13. Katibu wa Chama cha Soka Tabora, Fateh Rehmtullah amefungiwa maisha.

14. Mwenyekiti wa Chama cha Soka GEita, Salum Karunge ameachiwa.
15. Katibu wa Polisi Tabora, Alex Kataya ameachiwa huru, hakukutwa na hatia.
16. Mwamuzi wa akiba katika mechi kati ya Polisi Tabora Vs Oljoro, Hamisi Machunde amefungiwa miaka 10 na faini ya Sh milioni 10.

17. Mtunza vifaa wa Polisi Tabora, Boniface Komba pia ameachiwa huru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV