April 18, 2016
Dakika chache baada ya Washindi wa “Kwea Pipa Kwenda Spain na Azam Sports HD”, kuetua katika mji wa La Coruna, wamekutana bonge la "suprise" baada ya kukabidhiwa jezi za Derpotivo la Coruna zenye majina yao.

Washindi Ismail Salim na Jamal Mussa wametua mjini la Coruna baada ya safari ya zaidi ya saa 24 wakipita katika miji ya Zurich, Uswiss na Madrid, Hispania katika ya kufika hapa la Coruna.


Mara baada ya kutua, La Liga ambao ni wenyeji wao waliishajiandaa na kuwakabidhi jezi hizo orijino zikiwa na majina yao.

Jezi hizo watazivaa uwanjani kesho wakati watakapopata nafasi ya kushuhudia Live mechi la La Liga kati ya wenyeji Derpotivo la Coruna na wageni Barcelona ambao wanatua mjini hapa, kesho.

Pamoja na jezi hizo, washindi hao pia wamekabidhiwa jezi orijino za Barcelona.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV