April 2, 2016


Coutinho alitangulia kuifungia Liverpool iliyokuwa nyumbani Anfield, lakini Harry Kane akasawazisha na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Spurs ambayo ilipania kushinda lakini pointi moja inaifanya ifikishe pointi 61 ikiendelea kubaki katika nafasi ya pili.

Hata hivyo, kuanzia kocha na wachezaji wa Spurs walionekana kutofurahia sare hiyo, kwani sasa kama watapoteza mchezo mmoja na Arsenal kushinda, basi watakuwa wamejiweka katika hofu ya kung’olewa katika nafasi hiyo ya pili, jambo ambalo wasingependa liwatokee.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV