April 19, 2016Na Saleh Ally, Coruna
Washindi wa “Kwea Pipa Kwenda Spain na Azam Sports HD” leo wameweka baraka kwenye Uwanja wa Raizor ambao Derpotivo la Coruna kesho inaikaribisha Barcelona, wao wakiwa uwanjani hapo.

Washindi Ismail Salim na Jamal Mussa wamefaya ziara kwenye uwanja huo wakiongozana na washindi wengine kutoka Hong Kong na Sweden na kuangalia maandalizi ya uwanja huo kabla ya kesho mechi.

Hata hivyo, hakuna aliyeruhusiwa kukanyaga au kuugusa uwanja, hasa kwenye sehemu ya kuchezea na huo ni utaratibu wa uhakika.


Imeelezwa kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa na mwonekano bomba kabisa kabla ya mechi. Pia inasaidia mwonekano mzuri wakati utakapokuwa ukionekana kwenye runinga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV