April 18, 2016

Reinhard Grindel
Jamal Malinzi
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametumia salamu za pongezi, Reinhard Grindel kwa kuchaguliwa rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Ujerumani (DFB).

Katika salamu zake kwenda DFB, Malinzi amempongeza Grindel kwa kuchaguliwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi ambao hakuwa na mpinzani, na kusema hiyo imeonyesha imani ya watu wa Ujerumani dhidi yake katika maendeleo ya mpira wa miguu duniani.

Aidha Malinzi amesema TFF itaendelea kushirikiana na DFB chini ya uongozi wake Grindel katika shughuli za kila siku za maendeleo ya mpira wa miguu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV