April 20, 2016


Habari nzuri kwa mashabiki wa Bayern Munich, Manuel Neuer ni kuwa kipa wao wamesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo mpaka mwaka 2021.

Neuer, 30, alijiunga klabuni hapo akitoka Schalke kwa euro milioni 30 mwaka 2011 na tangu hapo ameshinda mataji matatu ya Bundesliga na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2013.

Kipa huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani alikuwa akihusishwa kuwaniwa na Manchester City, klabu ambayo kocha wake wa sasa, Pep Guardiola atatua msimu ujao.
Inaelezwa kuwa mkataba huo wa sasa utamwezesha kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri kikosini hapo akiwa sawa na mshambuliaji Thomas Muller ambaye analipwa euro milioni 15 kwa mwaka.

Mkataba uliokuwepo kabla ya huo wa sasa wa Neuer ulikuwa ukimalizika mwaka 2019.

Kipa huyo mpaka sasa ameshacheza mechi 313 katika Bundesliga akiwa katika timu zote za Schalke na Bayern.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV