April 20, 2016

MAYANJA
Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amewaomba radhi mashabiki na wadau wa Simba kutokana na timu hiyo kupoteza michezo miwili ya Ligi Kuu Bara na ile ya Ligi Kuu Bara.

Mayanja amesema kuwa bado anaamini timu yake inao uwezo wa kufanikiwa katika ligi kuu na ikiwezekana kutwaa ubingwa kutokana na kuwa lolote linaweza kutokea kwa vinara wa ligi kuu, Yanga.

Mayanja amezungumza hayo leo mchana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Simba zilizopo katika Jengo la Raha Tower jijini Dar ambapo alisema kilichotokea ni sehemu ya mchezo na kuwataka kutokata tamaa.

MAYANJA

“Mashabiki wa Simba hawatakiwi kukosa amani na tunawaomba radhi kwa kilichotokea, nia yetu ilikuwa ni kutwaa ubingwa wa Kombe la FA pamoja na Ligi Kuu Bara lakini imetokea tumetolewa kwenye FA.

“Hivyo nguvu zetu zote tunazielekeza katika ligi kuu kwa kuwa tunaimani lolote linaweza kutokea ikiwemo Yanga kupoteza pointi kisha sisi kushinda na kuwa mabingwa,” alisema Mayanja.


Wakati huohuo, nahodha wa timu hiyo, Musa Mgosi ambaye alikuwa pamoja na Mayanja alifunguka:

“Mashabiki hawatakiwi kukata tamaa sisi tutaendelea kupambana, wale wanaosema waachiwe Simba yao, hivi wanaweza kuiendesha klabu kweli? Klabu inahitaji mambo mengi kuiendesha, nafikiri huu ni muda kuwa na umoja na siyo kukwaruzana," alisema Mgosi.

KIKOSI CHA YANGA

1 COMMENTS:

  1. Hahahahahaha!waachieni simba yao jamani.
    Bado vichapo 2.Nasema na wewe Mayanja "DUA LA KUKU HALIMPATI MWEWE"

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV