April 20, 2016

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’ na straika Amissi Tambwe wamesema hakuna litakalowazuia kutosonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwani wana kikosi imara.

Leo usiku Yanga inacheza na Al Ahly mechi ya marudiano ya michuano hiyo baada ya hivi karibuni kutoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam.

Cannavaro ambaye yupo Misri akiwa na kikos chake hicho amesema Yanga iko imara na kwa upande wa ulinzi wapo vizuri wakitumia mfumo mpya wa 3-5-2 ambao mabeki watatu huanza kikosi kimoja.


“Tupo vizuri kuwatoa Al Ahly, tunajua hii ni timu kubwa lakini tutapambana kuhakikisha tunashinda na kocha tayari ametupa mfumo mzuri wa kujilinda na kushambulia kwa kasi,” alisema Cannavaro.


 Kwa upande wake, Tambwe alisema kimsingi kikosi chao kipo imara na kilichobaki sasa ni kuingia uwanjani kucheza kwa kujituma tu.

“Tunacheza na timu kubwa Afrika lakini hata sisi ni timu kubwa ndiyo maana tumefika hatua hii ya kuwania kufuzu hatua ya makundi, wote tupo sawa na tutapambana,” alisema Tambwe.


Yanga ikifanikiwa kusonga mbele itaingia hatua ya makundi na kama ikitolewa itakwenda kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kuwania kufuzu hatua ya makundi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic