April 21, 2016

IKICHEZA kwa kujiamini na kutawala mchezo, Arsenal imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Brom huku mashambuliaji wake, Alexis Sanchez akionyesha kiwango cha juu.

Pamoja na ushindi huo Arsenal ilicheza mchezo huo ikiwa na upungufu wa mashabiki ambapo Uwanja wa Emirates haukujaa kama ilivyokawaida yake kutokana na mashabiki kususia kiaina mchezo huo kama walivyosema mapema wiki hii.
Arsenal ambayo kwa ushindi huo imefikisha pointi 63 na kurejea katika nafasi ya tatu ya msimamo huo ikiishusha Manchester City iliyokuwa juu kabla ya mchezo huo wa jana usiku kwenye Uwanja wa Emirates, imerejesha matumaini ya kupambana kuwania ubingwa au nafasi mbili za juu katika mechi nne zilizosalia.

Sanchez ambaye katika mechi nane zilizopita amehusika kwa katika mabao 9 ya timu yake kwa kufunga sita na kutoa asisti 3, alianza kufunga katika dakika ya 6 kisha kuongeza la pili katika dakika ya 38 kwa kupiga faulo nzuri kutoka nje ya eneo la 18 iliyojaa wavuni moja kwa moja.

Matokeo hayo yanaifanya West Bromwich Albion kuendelea kubaki katika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 40 nayo ikiwa imesaliwa na mechi nne kumaliza msimu kama ilivyo kwa Arsenal.

Michezo ya Arsenal iliyosalia katika ligi hiyo ni dhidi ya Sunderland, Norwich City, Manchester City na Aston Villa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV